IMG_8978
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. George Simbachawene akiwa na wajumbe wa Bodi ya NHC na Watendaji wa NHC walipotembelea mji wa Bunggol wenye nyumba za wananchi (social housing estates) nchini Singapore kama sehemu ya ziara ya mafunzo.(Picha na Muungano Saguya-NHC)
IMG_9018
Ujumbe wa Tanzania ukielezwa namna mji wa Singapore ulivyopangwa kulingana na matumizi mbalimbali ulipotembelea Mamlaka ya Uendelezaji Miji ya Singapore(URA) jana. IMG_9034
Ujumbe wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukiwa katika Bodi ya Uendelezaji wa nyumba ya Singapore ambayo harakati za Bodi hiyo zimewezesha asilimia 86 ya watu wa nchi hiyo kupata nyumba za kuishi. Nchi ya Singapore ina watu milioni 5.4 IMG_9073
Ujumbe wa Naibu Waziri ukiwa katika kampuni inayosambaza na kusimamia usalama wa maji katika nchi ya Singapore na maeneo mbalimbali Tanzania ya Hyflux Innovation Centre ambayo pia imeonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania kusambaza maji katika maeneo inayojenga nyumba za wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2014

    Mrudi mje muendeleze makao makuu ya mikoa yetu ili ipanuke ikiwa imepangwa vituri.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2014

    NHC inaweza kupanuka zaidi pia ikitegemea zaidi wananchi wachangie kwa kununua nyumba zaidi wakati zikiwa kwenye michoro ya NHC na taasisi zinging za ujenzi wa makazi. Bei nafuu inayopatikana itaiongezea NHC mtaji wa ujenzi na nakuwa motisha kwa wananchi kuchangia makazi bora.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...