Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Mheshimiwa Chiku Gallawa atakuwa mgeni rasmi katika shindano la kumsaka mrembo wa mkoa huo, Nice & Lovely Miss Tanga 2014 siku ya jumamosi tarehe 21/06/2014, shindano ambalo litafanyika Mkonge Hotel.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mac D Promotions ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Irene Rweyunga amesema kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga amekubali kuwa mgeni rasmi, napia amepongeza maandalizi makubwa yaliyofanyika katika kuliandaa shindano hilo ambalo limekuwa gumzo katika jiji la Tanga.
"Tumedhamiria kulifanya shindano hili kuwa na msisimko wa kipekee, na maandalizi yote yamekamilika kwa asilimia mia moja nasasa tunasubiria siku ifike ili kumpata mshindi, alisema Irene.
Warembo wote 13 hivi sasa wapo kambini katika Hoteli ya Tanga Beach Resort chini ya mwalimu wao Mariam Bandawe na wanaendelea vizuri na mazoezi yao.
Mshindi wa kwanza wa shindano hilo atazawadiwa zawadi ya gari dogo aina ya Toyota Vitz ambalo tayari limeshapelekwa mkoani Tanga karibu wiki tatu sasa.
Shindano hilo ambalo liedhaminiwa na Nice & Lovely, EATV, Tanga Beach Resort, Breeze Fm, CXC Africa, Rweyunga Blog na Mwambao Fm, burudani kabambe itaporomoshwa na Malkia wa mipasho Afrika Mashariki, Bi Khadija Omary Kopa.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Mheshimiwa Chiku Gallawa |
Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014
Kumekucha Tanga
Warembo wakiwa na Toyota Vitz lmshindi wa kwanza mjini Tanga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...