Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya
(kulia) akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vyenye thamani ya
milioni 5/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulelea watoto waliokatika
mazingira magumu cha Irishad Madrasah cha Mbezi kwa Msuguri (kutoka
kushoto), Mkurugenzi wa Kituo, Ustadhi Maulid Salim Kidebe, Ayoub
Idrissa na Ramadhan Ayoub, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es
Salaam jana. Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza
kutoa futari kwa vituo vitano vinavyolea watoto hao vya Sharif Saidi Al -
Bath cha Mwanza, Al- Hidaya Children's Home cha Ilala, New Hope Family
cha Mjimwema Kigamboni na Kiboa Orphanage Arusha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya
(kulia) akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vyenye thamani ya
milioni 5/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulelea watoto waliokatika
mazingira magumu cha New Hope Family cha Mjimwema Kigamboni (kutoka wa
pili kushoto), Mlezi wa Kituo, Merry Stromberg, Victor Mshan, Anthony
Mtatiro na Mwenyekiti wa kituo, Omari Kombe, katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam jana.
Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa
jamii imeanza kutoa futari kwa vituo vitano vinavyolea watoto hao vya
Sharif Saidi Al - Bath cha Mwanza, Al- Hidaya Children's Home cha Ilala,
Irishad Madrasah cha Mbezi kwa Msuguri na Kiboa Orphanage Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...