Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Joyce Mapunjo akizungumza na moja ya chombo cha habari wakati
wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
ambaye ni Msemaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Vedastina Justinian
akimsikilia mwananchi aliyetembelea banda la wizara hiyo kwenye maadhimisho ya wiki
ya Utumishi ya Umma yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.Picha na
Hussein Makame-MAELEZO.
============ =========
Hussein
Makame-MAELEZO.
WAKATI Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki
walipotia saini Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1999,
kila upande ulilenga maslahi ya kiuchumi na maendeleo kwa nchi na wananchi wake
katika nyanja mbalimbali. Lakini ni ukweli ulio wazi kwamba
mafanikio ya nchi katika jumuiya hiyo hutegemea kwa kiasi kikubwa na ushiriki
wa wananchi katika hatua za mtanagamano huo kwani wao ndio walengwa wakuu
katika mchakato huo.
Ni miaka 14 imepita tangu wakuu wa nchi
za Afrika Mashariki waliposaini Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika
Mashariki na miaka 9 tangu kuanza kwa utekelezaji wa hatua ya kwanza ya
mtangamano wa jumuiya hiyo. Pamoja na mafanikio ambayo Tanzania
imeanza kuyapata kutokana na hatua mbalimbali za mtangamano wa jumuiya hiyo,
inaelezwa kuwa bado mwitikio wa wananchi katika kuchangamkia fursa zilizopo uko
chini.
Msemaji wa Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Vedastina Justinian anasema baada ya maandalizi ya miaka
sita, nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo zilianza kutekeleza rasmi hatua ya
Umoja wa Forodha mwaka 2005.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...