Na Sultani Kipingo
Bao la dakika ya nane
lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain lilitosha kuipeleka
Argentina kwenye nusu fainali za Kombe la Dunia walipocheza dhidi ya Ubelgiji
ambayo ilishindwa kabisa kuonesha cheche zake leo jijini Brasilia.
Higuain
alitumia vyema kosa la kizembe la nahodha wa Ubelgiji Vincent Kompany kuipaisha
Argentina kwa jaribio lao la kwanza kwenye goli la adui.
Kompany
aliupoteza mpira na Lionel Messi akauzima kabla ya kumtilia pande Angel Di Maria
upande wa kulia, na nyota huyo wa Real Madrid alibahatika pale pasi yake
ilipomgonga beki wa Ubelgiji Jan Vertonghen, na mpira ukajipeleka mbele ya
Higuain ambaye hakufanya makosa. Pichani Di Maria na Higuian wakimshukuru Messi ambaye pande lake lilizaa goli lao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...