Na John Gagarini, Kibaha
Kabla ya kumwua mtuhumiwa alikuwa akinywa pombe za kienyeji na marehemu lakini aliwahi kuondoka eneo la kinywaji kisha kumvizi marehemu na kumfanyia vitendo hivyo ambavyo vilisababisha kifo chake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani, kamanda mwandamizi msaidizi wa jeshi la polisi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo limetokea Kijiji cha Mfuru Kivukoni wilayani humo.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo Julai 10 mwaka huu majira ya saa 1:30 usiku Kijijini hapo ambapo mtuhumiwa alimvizia marehemu kwenye eneo la kichaka kisha kufanya unyama huo.
Katika tukio lingine Nuran Hamis (31) anashukiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma ya kusafirisha bangi kilo 12 akiwa kwenye basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili namba T 618 CMU.
Kamanda Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jana majira ya saa 2:00 usiku kwenye kizuizi cha Maliasili cha Kibiti kata na Tarafa ya Kibiti wilayani Rufiji.
Aidha watu watano wakazi wa Kidongo Chekundu kata ya Magomeni Tarafa ya Mwambao wilaya ya Bagamoyo wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kukutwa na pombe ya Moshi maarufu kama Gongo lita 21 kwenye matukio tofauti.
Aliwataja wathumiwa hao kuwa ni Hadija Shaban (37), Rajabu Michael (37), Msafiri Ramadhan (38), Seif Omary (35), Asha Ramadhan (40) pia wakazi watatu wa Ikwiriri wilayani Rufiji nao walikamatw awakiwa na lita 4 za pombe hiyo ambao ni Tabia Salehe (31), Hamis Rwambo (27) na Abdul Rwambo (40).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...