Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Tamasha la Mkoa wa Mtwara, ‘Mtwara Festival’,
linatarajia kufungua milango ya fursa kwa wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi
katika kuziona fursa kadhaa kwenye sekta ya Utalii na Uchumi.Tamasha hilo
linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia mwezi Agosti 16 na 17 mwaka huu
kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona ulipo
Mtwara mjini. Mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda huku likiwa na kauli mbiu isemayo ‘Fursa Zimefunguka, Tuzitambue,
Tujiandae, Tuzichangamkie.
Tamasha hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania Creative
Industries Network (TACIN) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
huku likisaidiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Akizungumzia Tamasha hilo
Mwenyekiti Mtendaji wa TACIN, Anic Kashasha alisema kuwa mikoa hiyo inautajiri
mkubwa katika utalii, uchumi na vivutio vingi mbalimbali.
"Mikoa hiyo ina utajiri mkubwa tena sana katika rasilimai zake
mbalimbali kama vile fukwe nzuri na za kuvutia, utajiri mkubwa wa historia yake
utamaduni na hata ubunifu wa aina mbalimbali hivyo matamasha kama haya
yanasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza utajiri huo," alisema Kashasha. Aliongeza
kuwa, "Kwa sasa mikoa hiyo imeghunduliwa kuwa ina utajiri mkubwa wa gesi
na hivyo kuna watu mbalimbali wameshaajiliwa ikiwa pamoja na kupatikana kwa
fedha nyingi tayari kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake na taifa zima kwa
ujumla."
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu
ya TTB, Devota Mdachi alisema kuwa utalii umekuwa kwa kiasi kikubwa
ukisaidia maendeleo ya uchumi wa nchi. Anasema kuwa katika tamasha hilo ambapo
kutakuwa na shughuli mbalimbali za kiutamaduni, sanaa na nyinginezo ni nafasi
kubwa ya kukuza utalii pia hasa utalii wa ndani au utalii wa kiutamadunia. "Ni
nafasi kwao katika kutangaza mengi kuhusiana na masuala ya Utalii, hapa nchini
au hata utai wa shughuli za kiutamaduni pia ni muhimu na hii ndio nafasi ya kipekee
kwao na kwa wadhamini mbalimbali kujitokeza kuunga mkono Tamasha hili la aina
yake," alisema Mdachi.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Ofisa ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Mkuu wa
Wilaya wa Mtwara na Mikindani Baraza la Wilaya la Mtwara Vijijini, Baraza la Biashara,
KIlimo na Viwanda (TCCIA). Wengine ni Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)
Pride FM, Radio of Mtwara pamoja na Kampuni ya Mawasiliano ya Strictly
Communications.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...