Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya
kujitambulisha, kuangalia fursa na wigo wa kuanzisha mahusiano mazuri kati ya nchi yake na Hospitali hii.
Dkt. Mohammed amesema kuna
Wacomoro wengi ambao wanapata huduma za tiba Hospitalini hapa hivyo ameona kuna haja na umuhimu wa pekee kuwa na uhusiano wa
kiutendaji rasmi ili Watalaam kutoka Komoro waje kujifunza na kupata uzoefu wa utoaji huduma za tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi. Agnes Mtawa.
Mh. Balozi akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mh. Balozi akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili mara tu baada ya ziara yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...