Pichani ni Meneja wa Tawi lililopo ndani ya maonyesho ya biashara ya Kimataifa
ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar,Bi.
Upendo Tendewa akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki
hiyo.Bi.Upendo amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kukidhi mahitaji ya
wateja ya kibenki na ya kifedha kwa kuhakikisha upatikanaji wa bidha na
huduma bora kabisa katika soko kwa bei inayowezekana kulipa na viwango
vyenye manufaa yanayolingana na gharama na faida ya kurudhisha kwa
mwanahisa.
Amesma benki hiyo inatumia kadi yako iitwayo Twiga ExpressCard ambayo mteja anaweza kuitumia kupata huduma za kibenki katika ATM yoyote iliyounganishwa na mtandano wa UMOJA SWITCH,ambapo zaidi ya ATM 180 na mabenki ishirini nna nne nchini yameunganishwa.
Afisa Masoko wa Benki ya Twiga Bancorp Bwa.Adalbert Alchard akizungumza
na Wanahabari nje ya banda lao kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo
na benki hiyo kwa wateja wao, kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa
ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar.Pichani kushoto ni Afisa wa Benki hiyo,Bi Tuddy Lutengano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...