Mwananchi (kulia) akiwauliza maswali wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania(kushoto)  juu ya huduma mbalimbali za Benki hiyo leo jijini Dar es salam wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Tasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA )Mzee Boma(wa pili kulia) akisaini Kitabu cha wageni leo jijini Dar es salaam wakati yeye na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) DKT. Joseph Kihanda (kulia) walipotembelea  Banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya  38 ya Kimataifa ya Biashara. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa TIA Lilian Mpanju(kushoto) na Mhasibu wa TIA George Kadutu.
 Mhasibu kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) George Kadutu akiwaelimisha wanafunzi wa Shule za Sekondari mbalimbali leo jijini Dar es salaam juu ya shughuli za Taasisi wakati wa maonesho ya  38 ya Kimataifa ya Biashara.
  Watumishi wa kutoka Mfuko wa Pesheni kwa Watumishi wa Umma (kushoto) wakitoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliotembelea banda la Wizara ya Fedha leo jijini Dar es salaam juu ya shughuli za Mfuko huo wakati wa maonesho ya  38 ya Kimataifa ya Biashara.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) DKT. Joseph Kihanda (kulia) akibadilishana mawazo na Wafanyakazi wa TIA kwenye Banda la Wizara ya Fedha leo wakati alipotembelea maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara. Wengine ni mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TIA Mzee Boma(wa pili kulia) , Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano Lilian Mpanju(kushoto) na Mhasibu wa TIA George Kadutu.
PICHA NA GCU- WIZARA YA FEDHA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2014

    Mmetokelezea, banda lenu zuri na nimeelimika vya kutosha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...