Mtu mmoja amethibitishwa kufariki Dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya baada ya moja ya Barabara
iliyokuwa kwenye matengenezo kukatika katika mji wa Belo Horezonte karibu na eneo lenye shughuli
nyingi la Lagoa da Pampulha,nchini Brazil.
Barabara
hiyo ipo kilometa 3 kutoka Mineirao
Stadium,uwanja uliotumika kwa mechi mbali mbali za kombe la dunia na
utatumika kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.
Barabara hii ilikuwa ni moja ya
kiungo kinachounganisha uwanja wa mpira na uwanja wa Kimataifa wa
Ndege. Barabara hiyo ni mpango wa mbasi ya mwendo kasi ambayo
ilisemekana ingekuwa tayari kutoa huduma wakati wa mashindano ya Kombe
la Dunia.

Maafisa
wa kikosi cha uokoaji nchini humo wamethibitisha kwamba Dereva wa basi hili ndie aliefariki Dunia katika
tukio hilo ambapo Barabara hiyo ambayo ni ya Juu (Fly Over) ilianguka kwenye mji wa Belo Horizonte.
Roli likiwa limekandamizwa na barabara iliyoanguka kwenye mji wa Belo Horizonte Julai 3,2014.(Picha zote kwa hisani ya Pedro Duarte / AFP/Getty Images)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...