Mwana wa Mfalme wa Japan Prince Akishino na mkewe Princess Kiko leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuona jinsi inavyotoa huduma zake kwa Watanzania. 

Akitoa salamu za pongezi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa amesema Hospitali imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA katika maeneo mbalimbali ya huduma ikiwemo ujenzi wa maabara maalumu ya watoto, ujenzi wa Kituo cha Maelezo ya Afya Muhimbili pamoja na kuongeza uwezo wa Hospitali katika kuboresha huduma zake kupitia mpango wa uboreshaji huduma (quality improvement program). 

Katika ziara yao, wametembelea Jengo la watoto kitengo cha watoto walioungua moto, wodi ambazo zimekidhi viwango vya ubora wa huduma, na jengo la wazazi ili kuona namna ambavyo akina mama wanapata huduma za afya ya mama na mtoto.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa akisalimiana na Prince Akishino wakati alipowasili Hospitalini hapo. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Dkt. Mahadhi Juma Maalim.
Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko wakifurahia jambo katika mojawapo ya wodi za watoto ambazo zimekidhi viwango vya program ya uboreshaji wa huduma.
Mkuu wa Idara ya Afya ya Akina Mama Dkt. Mathew Kallanga akitoa ufafanuzi kwa Prince Akishino kuhusu idara yake inavyowahudumia akina mama.
Princess Kiko akifurahia na akina mama baada ya kuona mtoto aliyekuja kliniki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2014

    One uses less muscles laughing, than frowning.
    Angalia katoto na mamake walivyofurahi na kucheka pamoja na wageni wetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...