Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokewa na Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC Tanzania, William Kallaghe na Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Mussa Assad (kulia) alipoalikwa kama mgeni rasmi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC Tanzania, Dk. Mussa Assad (wa pili kushoto) wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (wa pili kushoto) Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale (kushoto), wafanyakazi na wateja wa benki hiyo wakijumuika pamoja katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu ( kushoto) akiwaongoza baadhi ya wateja wa benki hiyo kushiriki futari waliyowaandalia jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali na kuwa karibu wateja wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2014

    Heee! NBC ina wateja wachache hivi??? au wametumia representative sample kama vile mambo ya rasimu.....

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2014

    Kiswahili kigumu sana, kuna neno BAADHI bwana hapo... so sijui picha ipi ingeweza kuwaweka wateja wao wote? du sura za watu zisingeonekana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...