Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akizungumza na Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Nditi, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za
CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo ya
Nditi wakati alipofanya ziara katika kata hiyo iliyopo Wilaya ya Nachingwea
mkoani Lindi. Waziri Chikawe alitoa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu
ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akimkabidhi jezi za timu
sita za mpira wa miguu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nditi, Patrick Mwasambungu kwa
ajili ya kuzikabidhi timu hizo zilizopo katika Kata hiyo katika Jimbo la
Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe pia alitoa mabati 100 kwa ajili ya
ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Mbunge huyo wa Nachingwea
yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM
katika ngazi mbalimbali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikiangalia kifusi
cha mchanga kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo
katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo,
Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa
Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na
viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (Kushoto), akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo
ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo,
Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa
Nachingwea yupo jimboni akifanya ziara
ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika Kata za Wilaya za Nachingwea mkoani
Lindi. Picha zote na Felix Mwagara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...