Na Woinde Shizza,Manyara

Wananchi wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kutumia fursa ya kuwepo kwa huduma ya benki ya CRDB Tawi la Babati, kwa kujiwekea akiba na kuchukua mikopo kwa lengo la kujinufaisha kiuchumi na kuongeza pato la Taifa.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo aliyasema hayo wakati wa zoezi la benki ya CRDB tawi la Babati, lilipoanza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake na yeye kuwa mtu wa kwanza kuweka fedha kwenye tawi hilo.

Mbwilo aliwataka wananchi wa mkoa huo kufungua akaunti za fedha kwenye benki tofauti ikiwemo CRDB, NMB, NBC, Posta na Exim, ambazo zipo mjini Babati, kuliko kuweka kwenye benki moja na kuitegemea yenyewe pekee.

"Waswahili wanasema usiweke mayai yote kwenye kapu moja, hivyo tutumie fursa hii kwa kuweka akiba katika benki tofauti tofauti, hapa unaweka sh200, kule sh300, pengine sh100 ndiyo nidhamu ya fedha ilivyo," alisema Mbwilo.

Hata hivyo, alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete mmoja wao ndiye atakayekuja kulizindua rasmi Tawi hilo na alitoa wito kwa benki hiyo ya CRDB kuanzisha matawi mengine kwenye wilaya za mkoa wa Manyara.

"Siku za nyuma tulikuwa tunaona gari la benki linakuwa hapa kwa wiki mara moja ila sasa mmeweza kuweka Tawi hapa Babati, sambaeni na sehemu nyingine huko wilayani msogeze huduma hizi karibu na jamii," alisema Mbwilo.

Naye, Meneja wa CRDB Tawi la Babati Ronald Paul aliwataka wafanyabiashara, watumishi, wakulima na wafugaji wa mkoa huo kutumia fursa ya kuwepo kwa benki hiyo kwa ajili ya kupata huduma za kifedha ikiwemo kuweka akiba.

"Jamii itumie nafasi hii kwa kuweka na kutoa fedha na pia hapa Babati ni kwenye barabara kuu hata viongozi wengi wanapita kuelekea Dodoma, hivyo watatumia fursa hii ya kuwepo kwa tawi letu kupata huduma ya fedha," alisema Paul.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mkoa huo, wakiwa kwenye Tawi la Babati la Benki ya CRDB ambalo jana lilianza kutoa huduma kwa wateja wake, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Khalid Mandia, akifuatiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndeng'aso Ndekubali na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Omary Chambo na Meneja wa Benk ya CRDB Kanda ya kaskazini Chiku Issa.
Meneja wa Benki CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, Ronald Paul akizungumza na waandishi wa habari ambapo kwa mara ya kwanza Tawi hilo.
Afisa wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara akitoa maelezo ya kibeki kwa baadhi ya Askari wa Jeshi la Wanzanchi waliofika kwenye Benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...