Filamu Mpya ya Cultural Wars Sasa Yapatikana! Wahi Kujipatia DVD! 


Ile filamu mliyokuwa mnaisubiri kwa hamu iitwayo “Cultural Wars” iliyoandikwa na kutengenezwa na Deogratius Mhella (Mtanzania anayeishi New York) akishirikiriana na Watanzania na Wamarekani waishio New York, New Jersey Boston na Connecticut sasa imetoka kwa mara ya kwanza na inapatikana kwenye DVD na unaweza kupata “electronic Copy” 
Filamu hii inazungumzia baadhi ya changamoto za kimapenzi wazipatazo vijana wa Kitanzania hapa Marekani. Na ni ya kwanza iliyochezwa na Watanzania na Wamarekani hapa New York kwa kutumia lugha ya Kiingereza. Baadhi ya “Actors” wa Kitanzania ni Khalifa Siwa aka “Bob”,  Ny Ebra aka “Vijimambo New York”, Akida aka “Mshenga”, Chemi Whitlow aka “Chemponda” na Isaac Kibodya aka “Father”. Wote mliosaidia katika kufanikisha filamu hii ambao hamjatajwa hapo juu, mnapewa shukrani za dhati kabisa. 




Usikose kujipatia nakala yako kwa kuinunua hapa chini: 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...