Na Francis Godwin Blog.
DIWANI wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kata ya Lupingu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe John Kiowi amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa jitihada zake anazozifanya katika kuwapelekea maendeleo wananchi wa Ludewa huku akiwashangaa wapinzani wanaopinga jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM) na kudai kuwa yeye si mpinzani wa uchwara wa kupinga maendeleo .
Akizungumza na wanahabari jana wakati wa zoezi la mbunge Filikunjombe na diwani huyo kushiriki na wananchi wa kata ya Lupingu kuchimba mashimo ya nguzo za umeme na kusimika nguzo hizo za umeme , Kiowi alisema kuwa ni zaidi ya wabunge watano wamepata kuliongoza jimbo hilo la Ludewa ila ni mara yake ya kwanza kuona mbunge akishiriki bega kwa bega na wananchi wake kuchimba mashimo kama ambavyo mbunge huyo anafanya .
" Jamani wananchi kwanza ni jambo la kumpongeza mbunge wetu mbali ya kuhimiza wananchi ila mwenyewe pia amekuwa mstali wa mbele katika kushiriki tofauti na wana siasa wengine ambao muda wote wao ni watu wa majukwaani ila vitendo sifuri .....nasema Ludewa imempata mbunge na niweke wazi hapa mimi sio mpinzani hivi tujiulize wenyewe nikisema mimi ni mpinzani napinga nini hapa haya maendeleo ni kwa faida yangu na wananchi wote sasa kama mbunge wa CCM wanafanya kuna haja ya upinzani hapa ".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...