Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifungua mkutano wa siku moja wa  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo siku nzima ya Alhamisi liLIjadili  ajenda ya uwekezaji kwa Afrika  na  mchango wake kwa Maendeleo endelevu. Katika hotuba yake,  Ban Ki Moon alisema  Afrika isiridhike na ukuaji  wa jumla wa uchumi wake ambao umekuwa ni mzuri bali inahitaji kuwekeza zaidi  ili uwekezaji huo uweze kuchangia katika kuleta maendeleo endelevu,  kuwaondolea  watu wake umaskini, kukuza ajira na kipato na  kwamba Afrika ilihitaji kuwekeza zaidi katika miundombinu,  kilimo na nishati endelevu pamoja na mambo mengine.

Muwakilishi wa Kudumu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Tuvako  Manongi akizungumza wakati wa mkutano kuhusu uwekezaji katika Afrika.  Katika mchango wake, alisisitiza kuwa  pamoja na Afrika kuchagizwa kuvutia uwekezaji zaidi pamoja na ukusanyaji wa mapato ya  ndani   Jumuiya ya kimataifa  inatakiwa kutoa ushirikiano  usio na shaka katika udhibiti wa ukwepaji mkubwa wa kodi, utoroshwaji  na biashara harafu ya fedha  na ambayo  inazinyima nchi za Afrika mapato ambayo yangeweza kutumika katika  utekelezaji wa miradi mbalimbali  ya maendeleo na hivyo kuwaondoelea  wananchi wake  umaskini  uliokithiri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...