Na Mwandishi Maalum, New York
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bw. Said Djinnit wa Algeria kuwa Mjumbe wake maalum atakaye shughulikia Eneo la Maziwa Makuu. 
Bwana Djinnit anachukua nafasi ya Bi. Mary Robinson wa Ireland, ambaye mapema wiki alimtangaza kumteua kuwa Mjumbe wake Maalum kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ( Climate Change) 
 Akitangaza uteuzi huo Ban Ki Moon, amemuelezea Bw, Djinnit kama mtu mwenye uzoefu mkubwa na ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa na katika Umoja wa Afrika. Na kwamba kutokana na uzoefu wake anamtarajia kutoa mchango mkubwa katika mchakato wa utafutaji wa Amani ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
Kuanzia mwaka 2008 hadi hivi karibuni, Bwana Djinnit amekuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Msimamizi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi. Pia amehudumu kama Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Katibu Mkuu nchini Nigeria,akisaidia juhudi za kupambana na Boko Haram. 
Djinnit ana uzeofu mkubwa katika masuala ya diplomasia, akiwa amewahi kuhudumu kama Kamishna wa kwanza wa Organi ya Usalama na Amani ya Umoja wa Afrika ( AU) na kabla ya kuzaliwa upya kwa AU, aliwahi Katibu Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Siasa katika OAU ( Organization of African Union) 
Wakati huo huo Katibu Mkuu pia amewateua Bw. Staffan de Mistura kuwa Mwakilishi wake Mpya kuhusu Syria atasaidiana na pia amemteua Bw. Ramzy Ezzeldin Ramzy kama makamu wake. 
 Bw. Staffan de Mistura anachukua nafasi ya Mwanadilomasia mzoefu na anayeheshimika Bw. Lakhder Brahimi aliyejiuzuru mwezi mei mwaka huu. Bw, Staffad de Mistura anakuwa Mwakilishi wa tatu kuteuliwa kushughulikia mgogoro wa Syria, wa kwanza alikuwa ni aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan ambaye naye alijiuzuru.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon akiwa  Bw. Said Djinnit wa Algeriaambaye amemtangaza kuwa  Mjumbe wake Maalum   atakayeshughulikia Eneo la Maziwa Makuu. Bw. Djinnit anachuka  nafasi ya  Bi. Mary Robinson wa Ireland ambaye hivi karibuni   Katibu Mkuu amemteua kuwa mjumbe wake katika masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  akiwa  katika picha ya pamoja wa Wawakilishi wake ambao amewateua kushughulikia mgogoro wa Syria kushoto kwa  Katibu Mkuu ni  Bw.   Staffan de Mistura   na kulia kwa Katibu Mkuu ni  Bw. Ramzy Ezzeldin Ramzy  ambaye  ni  Makamu wa Bw. Mistura. Bw. Staffan de Mistura anachukua nafasi iliyoachwa na Bw.  Lakhder Brahimi aliyejiuzuru mwezi  Mei

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...