Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, leo Julai 5, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Mbogamboga aina ya Kabeji ilivyostaawi katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kiatu aina ya Buti ambacho kimetengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Karanga Moshi, Kiwanda hicho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza. Rais Kikwete ametembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014  katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  Jijini, Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...