Wachezaji timu zote mbili wakisalimiana Rwamishenye FC vs Nshambya FC

Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Rwamishenye Fc leo imeifunga Nshambya mabao 4-0 kwenye mchezo wao wa pili LIGI YA KAGASHEKI. Mtanange wao wa kwanza wa Ufunguzi wa Hii Ligi waliwanyuka bao 3-1 Mabingwa watetezi Bilele Fc 3-1.
Rwamishenye waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na makeke ya wachezaji wake ilijikuta Mchezaji wake Hatari Khalid Seleman akifunga bao zote Nne. 

Kipindi cha kwanza Khalid Seleman aliifungia bao mbili na kufanya 2-0 dhidi ya timu ya Nshambya. Kipindi cha pili tena akafunga bao mbili bao moja likiwa la penati.
Mapema leo mchana timu ya Bilele Fc Mabingwa watetezi aliifunga bao 1-0. 
Mashindano haya yataendelea tena kesho na kwa mechi mbili, Mechi ya kwanza itakuwa ni Hamugembe Fc vs Bakoba Fc saa 8:00 mchana na jioni sa 10:00 jioni ni Kahororo vs Kashai.
Waamuzi wa Mchezo huo Pamoja na Manahodha wa Timu zote mbili wakiteta kabla ya kuanza kipute jioni hii.
Waamuzi wa Mchezo huo Pamoja na Manahodha wa Timu zote mbili kwenye picha ya pamoja.Kikosi cha timu ya Bodaboda Rwamishenye.
Kikosi cha Timu yaNshambya Fc.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...