Baadhi ya wajumbe wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakichukua baadhi ya Madawa ya kufanyia usafi ambayo taasisi hiyo imechangia katika wodi ya watoto katika hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam kuboresha usafi katika Hospitali Hiyo Kubwa Jijini Dar es Salaam.
Dr. Mohamed wa Wizara ya Afya, Mh. Asha Mtwangi Mjumbe Bunge Maalum la Katiba na Ndugu Hassan Swedi, Meneja wa Fedha BORDA – Tanzania wakisikiliza kwa makini taarifa ya Muuguzi wa zamu juu ya Changamoto za kuwaangalia watoto wenye matatizo mbali mbali na jinsi wanavyopambana nayo katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala – Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation Bw. Mohamed Kamilagwa akimfaraji Mmoja wa Wazazi wa Mtoto anayesumbuliwa na Malaria katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.
Mh. Asha Dodo Mtwangi akipata Maelezo kutoka kwa wazazi wa watoto waliolazwa katika hospitali ya Mwananyamala. Mh. Asha Mtwangi alifanya ziara hiyo asubuhi ya siku ya EID El Fitr pamoja na wajumbe wenzake wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation ili kuwafariji watoto na wazazi wa watoto katika Hospitali ya Mwananyamala – Dar es Salaam.
Mh. Asha Mtwangi akifurahi na mtoto mchanga aliyezaliwa usiku wa mkesha wa siku ya EID. Anayeangalia pembeni ni Bwana Hassan Swedi akiwa na Muuguzi wa Mwandamizi wa zamu wa Hospitali ya Mwananyamala wakati wa Ziara Maalum ya Kusheherekea Sikukuu ya Eid el Fitr.
Baadhi ya Wajumbe wa Kalamu Education Foundation wakitafakali mafanikio na changamoto za uendeshaji wa hospitali za Umma hasa kwa watanzania wa kipato cha chini wakati wa ziara ya wajumbe wa Taasisi hiyo katika Hospitali ya Mwananyamala Siku ya Eid el Fitr.
Jazakallahu kheir
ReplyDeleteAllah awalipe
ReplyDelete