Maofisi wa Magereza la Isangaa - Dodoma Afande Kapitukaa Pamoja na Afande Hassan wakikagua msaada wa chakula kutoka Taasisi ya Kalamu Education Foundation kama Mchango wao kwa wafungwa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Pamoja na Maofisa hao Kulia ni Dada Safia na Dada Amina kutoka taasisi hiyo.
Wajumbe wa Kalamu Education Foundation Dada Safia na Dada Safina Mara Baada ya Kutoa Shukran kwa Ushirikiano walioupata kutoka kwa Jeshi la Magereza kuhakikisha kwamba wafungwa wanakumbukwa na Jamii vipindi maalum hasa vya kiroho kwani wengi hupata faraja na kuona bado ni sehemu ya Jamii husika na huchangia kuhamasika kiroho na kuwa raia wema.
Allah awalipe, wafungwa nao wataweza kufunga vyema ramadhani yao in shaa Allah
ReplyDeleteMungu atawapa barka tele lkn kuna jambo naomba nichangie swadaka ilio bora ni ile utoe mkono wa kulia mkono wa kushoto usijui inshalah tujitahidi kutoa sadaka kwa ajili ya alah tusipende kile mtu ajue kama umetoa sadaka
ReplyDeleteJazakallahu Kheri... Allah awazidishie, mimi nawaunga mkono kutufahamisha hivi mana kila mtu anafuturisha ma kampuni kwenye mahoteli makuuubwa nakusahau ndugu zetu awalio kwenye dhiki. Sipingi mchango wako kuhusu Swadaka Bora ILA kwahili nimejifunza. Allahu Alam
ReplyDelete