Germany ndio mabingwa wa kombe la Dunia 2014 FIFA World Cup, wakinyakua kombe kwa mara ya nne katika historia yao baada ya kuwashinda Argentina 1-0 kwa bao la muda wa nyoingeza la Mario Gotze (pichani juu kushoto) katika uwanja wa Maracana huko Rio de Janeiro.
Mchezaji huyo aliyeingia kama mchezaji wa akiba aliweza kuua uwezekano wa kupigiana penati kwa bao lake la uamuzi baada ya timu hizo kutoka suluhu hadi mapumziko katika mchezo uliojaa kila aina ya msisimko. Bao lake hilo liliwamaliza kabisa Argentina ambao walishindwa kujibu mapigo, na Germany wakaongeza nyota ingine katika historia yao kufuatia ubingwa wao wa mwaka 1954, 1974 na 1990.
Wananchi wa Bagamoyo wakifuatilia mchezo wa fainali za kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo ambapo Germany ilifanikiwa kunyakua kombe hilo dhidi ya Argentina ya kina Messi
Hongera Ujerumani kwa kulitwaa kombe. Mwaka 2018 je kutakuwa angalau na timu ya Afrika Mashariki?
ReplyDeleteWalistahili kwanza wamecheza nusu fainali mbili na fainali mbili ndani ya miaka 12 pili wana kocha ambaye wamekaa naye nafkiri zaidi ya miaka 10 makocha wengi hawadumu kukaa na tim za taifa miaka yote tatu wanamchanganyiko wa wachezaji wana asili ya mataifa tofauti wameachana na zambi ya ubaguzi wa rangi na dini hongereni sana
ReplyDeleteWananchi wa Bagamoyo katika hili eneo hapo wanahitaji ukumbi bora zaidi wa kuangalia mpira..
ReplyDelete