Sheikh Suleiman Amran Kilemile Alipokuwa akifungua Kituo Cha Jamaat Islamiyyah Madrassa and Nursery School Cha Kisarawe. Sheikh Kilemile aliwahusia wazazi kuwasomesha watoto wao Masomo yote kwani husaidia kupata Viongozi Waadilifu na wenye Huruma katika Maendeleo ya Jamii.
Sehemu ya Majengo ya Kituo Kipya cha Masomo ya Awali Cha Jamaat Islamiyya Kisarawe Pwani.
Sheikh Suleiman Kilemile akiwa na Mbunge wa Kisarawe Mh. Suleiman Jaffu pamoja na watoto wa Wilaya hiyo wakionyesha Matumaini Mapya Baada ya Taasisi ya Kalamu Education Foundation Kukabidhi kituo Cha Jamaat Islamiyyah Madrassa and Nursery School Kisarawe.
Mh. Aisha Dodo Mtwangi (Wapili Kulia) akiwa Pamoja na Wajumbe wenzake wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakati wa Ufunguzi wa Kituo Cha Masomo ya awali. Wengine ni Maryam Abdulkadir, Neema Idd na Farida Mohamed.
Mgeni Rasmi Sheikh Suleiman Amran Kilemile akisindikizwa na Mbunge wa Kisarawe Mh. Suleiman Said Jaffu mara baada ya Uzinduzi wa Kituo Cha Masomo ya Awali na Elimu ya Dini wilayani Kisarawe Kilichojengwa na Kalamu education Foundation.
Baadhi ya Wajumbe wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakiwa pamoja na Viongozi Mbali Mbali wa Kidini wa wilaya ya Kisarawe wakati wa Uzinduzi wa Kituo Cha Elimu ya Awali wilayani hapo.
Hongereni sana kwa kazi nzuri,endeleeni kwa moyo huohuo na wengine watahamasika...
ReplyDeleteAllah awalipe kwa kazi yenu nzuri, Awajaze kila lililo la kheri duniani na akhera
ReplyDeleteJazakallahu kheir, Allah awazidishie na awawekee wepesi Katika yote
ReplyDeleteAlhamdulillah
ReplyDelete