2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko Moroco jijini Dar es salaam wakati akielezea kuhusu kukamilika kwa maadalizi ya uzinduzi wa albam ya mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando inayojulikana kama "Kamata Pindo la Yesu" maarufu FACEBOOK utakaofanyika kwenye ukumbi wa VIP Diamond Jubilee Agosti 3/ 2014 jijini Dar es salaam na kufuatiwa na maonesho mengine katika mikoa ya Tabora, Geita na Mwanza mara baada ya uzinduzi wa Dar es salaam, 
Msama ameongeza kuwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wamethibitisha kushiriki katika uzinduzi huo ambao ni John Lisu, Upendo Kilahiro, Upendo Nkone , Ephraim Sekereti na wengine wengi, Tiketi zinapatikana katika vituo vifuatavyo Maduka yote ya Msama Promotion Kariakoo na Posta, Bestbite Namanga, vituo vya mafuta Puma Mwenge na Airport. Watu wote mnahimizwa kuwahi kununua tiketi ili kujihakikishia nafasi katika uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...