Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bahati Bukuku akiwa kwenye moja ya kazi zake ya uimbaji.

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Gari lenye namba IT 7945 aina ya Toyota Nadia ikiendeshwa na EDSON S/O MWAKABUNGU, Mnyakyusa, Miaka 31 mkazi wa Tabata – Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeruhi kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari lingine linalosadikiwa kuwa ni Fuso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 majira ya saa 03:00 alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.

Kamanda MISIME amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni EDSON s/o MWAKABUNGU ambaye analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI D/O BUKUKU, Miaka 40, Mnyakyusa, Msanii wa nyimbo za Injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake na FRANK S/O CHRISTOPHER, Muha, Miaka 20, Msanii wa muziki wa Injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam yeye ana michubuko usoni na mkono wa kulia. Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Aidha Kamanda MISIME ameongeza kwa kusema kuwa watu walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.

Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2014

    kaka michuzi salaam kwanza jingine hili la kuweka makabila ya wahusika wa habari limeanza zamani au siku hizi kwa sababu miaka mingi nimesoma habari Tanzania sijapata kuona wala kusoma umuhimu wa kuweka kabila iwe kwa utambuzi au vinginevyo.
    mwalimu nyerere alituonya kwa kusema hivi na nanukuu.
    'mnaanza ukabila'
    hakuna madhara kuwatambua wahusika pia kwa makabila yao tatizo huu ndio mwanzo wa balaa kama hakuna umuhimu kabila lisitumike leo kwenye ajali kesho kwenye kutafuta ajira au mchumba baadae katika kupandishwa cheo nafikiri umepata ninakoelekea.
    shukrani.
    mdau
    mgogo kwa mama/baba hajulikani kabila lake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2014

    Mdau wa kwanza hapo nimeona wasiwasi wako! Ila kwa upande wangu sioni tatizo. Hii inatokana na vita batili tuliyokuwa nayo hapo awali ya kupambana na ukabila kwa ku-demonize (kwa Kiswahili sijui kutukana) makabila yetu. Lakini wengine tukiwatambua kwa makabila yao haionekani kama ni ubaguzi: mfano waZulu, baCongo, waKurdi, waTuruki, waRusi, waSomali, waAjemi, waShirazi n.k. Tatizo linakuja kwa makabila madogo ndani ya nchi. Lakini tusiogope, tuyazoee na iishie hapo, sio zaidi. Tujielimishe kwa mambo makubwa zaidi na makabila yatabaki tu kama identity (utambulisho) ambao hauwezi kufutika milele!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2014

    Hizo za kuandika makabilanadhani ni taratibu za kipolisi. Na hii habari imetolewa na jeshi la polisi. Habari nyingi za kimatukio huwa zinatolewa hivyo. Si kosa la Michuzi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2014

    As ante mdau hapo juu.kwa taarifa ya polis I ni lazima waandike full details zako ikiwemo makazi, miaka, Manila nk ili iwe rahisi kutambulika.tusipende kukimbilia kwenye negative bila kujua kwa nini imeandikwa hivyo.tupunguze lawama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...