Afisa
Biashara Mkongo wa Taifa wa mawasiliano,Bwa.Thomas Lemunge akielezea
kuhusiana na Mkongo wa Taifa wa mawasiliano unavyofanya kazi, mapema leo
ndani ya maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi sasa jijini Dar Es Salaam.
Bwa.Thomas
amebainisha kuwa Mkongo wa Taifa wa mawasiliano umekwisha sambaa maeneo
mengi ikiwemo mikoa 21 ya Tanzania mpaka sasa,Amesema kuwa Makampuni
yote ya ndani yanatumia mkongo huu wa mawasiliano kupeleka huduma kwa
wananchi na kuongeza kuwa Mkongo huo unaunganisha mataifa mbalimbali
kupitia mkongo huu wa Taifa wa Mawasiliano ambao umerahisisha mambo
mengi katika jamii ikiwemo suala zima la mawasialiano ya simu za
kiganjani na mambo mengineyo.
Bwa.Thomasa
amewataka wananchi kuhakikisha wanautunza na kuulinda Mkongo huo wa
mawasiliano ili kuendelea kurahusisha upatikanaji wa huduma mbalimbali.
Afisa
Mahusiano wa kampuni ya Simu ya TTCL-Tanzania,Bwa.Edwin Mashashi
akielezea kuhusiana na huduma zao mbalimbali zitolewazo na kampuni
hiyo,ikiwemo masuala ya Internet na huduma nyinginezo mbalimbali kwa
wateja wao.
Bwa.Edwin
ameeleza kuwa kwa sasa kampuni yao iko katika mchakato mkubwa wa
kuziboresha huduma zao ziwe na ubora zaidi,ameongeza kusema kuwa pia
Wanatarajia kufunga Wi-Fi katika maeneo mbalimbalu ya jiji la Dar,
ambapo gharama itakuwa ni ya bei nafuu.
Edwin amesema kuwa Kampuni ya TTCl-Tanzania,wanatarajia
kuzindua kituo kikubwa Afrika Mashariki cha kuuzia internet,kituo hicho
kinatarajia kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Julai ama Agosti,''mtambo
huo tayari umekwishafungwa hapa hapa nchini tayari kwa kuanza kutoa
huduma hiyo Afrika Mashariki,hivyo kutakuwa hakuna haja tena ya kununua tena Internet nje'',amedema Bwa.Edwin.
Pichani ni baadhi ya wateja wakipata maelezo maelezo mbalimbali kuhusiana na huduma zitolewazao na Kampuni ya simu TTCL,ndani ya banda la kampuni hiyo ndani ya maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi sasa jijini Dar Es Salaam.
Wahudumu wa TTCL wakihudumia wateja wao kwa njia ya simu ndani ya banda lao,katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hivi sasa jijini Dar Es Salaam.
Namna mkongo wa Taifa unavyofanya kazi na maeneo mbalimbali ulivyosambaa nchini.
their customer services is very poor and dont value their customers.Also they internet is not stable it keeps on resetting going down then up itself every now and then.Not stable
ReplyDelete