Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (wapili kulia) akitoka kwenye Banda la Wizara yake wakati
wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya
Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soko la Ndani, Edwin
Rutageruka na kulia ni Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Christina Mwangosi. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea
viwanja hivyo kuangalia hali ya usalama.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacquline Maleko akimfafanulia
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi
(IGP) Ernest Mangu (kushoto) na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Suleiman Kova (kulia) jinsi Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi walivyojipanga kuimarisha usalama katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa
Msafara wa Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mathias Chikawe wakizunguka katika viwanja vya Sabasaba katika Maonyesho
ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo
vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama
katika viwanja hivyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (wapili kulia) akikiangalia cheti cha usajili wa vyama katika
Banda la Wizara yake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya
Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la
Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam,
kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo. Kushoto ni Afisa Sheria, Flora
Mlope ambaye alikuwa akitoa maelezo ya usajili wa vyama. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...