Dotto Mwaibale
KITUO
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kuwa hadi kufikia Juni
2014 wanawake na wasichana 2878 wamebakwa nchini kutokana na vitendo vya
ukatili dhidi yao.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen
Kijo-Bisimba wakati akitoa taarifa ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia
Januari na Juni mwaka huu kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo.
"Vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya makundi hayo vilivyoripotiwa polisi kwa nchi nzima vilikuwa 3,633" alisema Kijo -Bisimba.
Kijo-Bisimba
alisema taarifa hii inatoka na tafiti zilizofanywa na kituo hicho ili
kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwa waangalizi wa haki
za binadamu, wasaidizi wa sheria, taarifa rasmi kutoka taasisi za
Serikali, Bunge, Mahakama,vyombo vya habari na asasi mbalimbali zisizo
za kiserikali.
Akizungumzia
kuhusu taarifa ya Sensa ya watu na makazi inaonesha idadi kubwa ya watu
wanaishi vijijini huku wakiwa na huduma duni za kijamii kama za afya,
maji, umeme, umeme na shule.
Alisema
takwimu zinaonesha bado vijijini kuna makazi duni ya wananchi kutokana
na gharama kubwa za saruji na vifaa vya ujenzi, mfano katika suala la
upatikanaji maji makazi 3,959,857 yanatumia vyanzo vya maji visivyo
salama ukilinganisha na makazi 1,902,244 yanayotumia maji ya bomba nchi
nzima.
Kuhusu
kilimo alisema idfadi ya wananchi wengi wapatao 11,359,090 wanategemea
kilimo kama shughuli kuu ya uchumi hata hivyo wakulima wengi bado
wanatumia jembe la mkono.
"Uwekezaji
katika mashamba makubwa wamepewa wawekezaji wakubwa mfano mashamba
makubwa ya mpunga yaliyokuwa ya Shirika la NAFCO wilayani Mbarali mkoani
Mbeya wamepewa wawekezaji na wakulima wazawa wametengewa yasiyofaa"
alisema Kijo-Bisimba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen
Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leoasubuhi, wakati akitoa taarifa ya kituo hicho ya
kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari hadi kufikia Juni 2014. Kulia ni
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na
Mtafiti wa LHRC, Pasience Mlowe.
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe (kushoto), akisoma taarifa hiyo kwa wanahabari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...