Mgombea wa Urais wa Jumuiya ya waTanzania DMV, Bwana Liberatus Mwang’ombe "Libe". (wapili kulia) akipata picha ya pamoja na  waumini wa  Tanzanian Muslim Community in  (TAMCO) Siku ya Jumapili July 6, 2014 ndani ya ukumbi wa Indian Spring ulipo Silver Spring Maryland

Na  Abou Sharty Washington DC 

 Mgombea wa Urais wa Jumuiya ya waTanzania DMV, Bwana Liberatus Mwang’ombe "Libe", siku ya Jumapili July 6, 2014 alipata fursa ya kujumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Tanzanian Muslim Community (TAMTCO), iliopo Washngton DC Metro,  kwaajili ya kuonyesha umoja na mshikamano dhidi ya Jumuiya ya mbali mbali ziliopo hapa DMV.

Bwana Liberatus Mwang’omb, alisema kua ''Alifurahishwa sana na kitendo cha ushirikianao huo wapamoja unaofanywa na Jumuiya ya waIslamu, kwa ushirikiano wao na  kupata futari ya pamoja pale ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao hukusanyika familia mbalimbali na kuweza kupata chakula cha pamoja, " nilijisikia nipo nyumbani na kuwa na furaha  na kila mmoja aliehudhuria katika futari hiyo'' alisema

Katika kampeni za uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV, zinazoendelea kwa kasi mjini hapa Bwana Liberatus Mwang’ombe, mwezi uliopita, siku ya jumamosi June 28, katika kiwanja cha Meadowbrook Park, alipata fursa ya kufanya mkutano wa sera zake za kuleta maendeleo kwa wakaazi wa Jumuiya ya waTanzania DMV, pindi atakapochaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya, katika mkutano huo aliweza kushirikiana na baadhi ya wagombea kwaajili ya kampeni za kuleta maendeleo dhidi ya waTanzania, waishio hapa DMV.

 Bwana Libe aliweza kuzungumzia kuhusu  marekebisho ya ubadilishaji wa vifungu vya katiba zinavyomkaba Mtanzania anaeishi hapa DMV, kulipa ada, ndipo apate fursa ya kupiga kura, alisema vifungu hivyo atakapochaguliwa atakuwa tayari kuviondoa, pale tu atakapokubaliana na wanajumuiya kutokana na kutowapa furasa watu waTanzania wanaoishi hapa DMV kutopiga kura hadi walipe ada na kuwa wanachama hai ndipo wapige kura wakiwa kma wazawa halisi wa Tanzania.

Mara baada ya ftari Bwana Liberatus Mwang’ombe alisema juu ya mfumo mzima wa ushirikiano wa kuendesha Jumiaya hiyo bila ya kujali itikadi ya mtu yoyote ile na kuwa kitu kimoja na kuonyesha umoja na mshikamano kwaajili ya kumnyanyua mTanzania alie hapa DMV, pamoja na kuitangaza nchi yetu Tanzania na kuwa wazalendo wa ukweli na wakujitolea pale mTanzania mara tu atakapofikwa na matatizo ya aina yoyote, aliongea hayo mara tu baada ya kuungana na iftar ya Tanzanian Muslim Community in Washington DC Metro (TAMCO) na huku akisisitiza kuomba kura zenu pindi mtakapolipa aida za upigaji kura zenu, na kumchagua kiongozi mnaemtaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...