Balozi wa Tanzania nchini Zambia,Mhe Balozi Grace Mujuma tarehe 2 Julai hadi 6 Julai 2014 alifanya ziara ya kikazi ya siku nne jimbo la Copperbelt mji wa Ndola. Katika ziara hiyo, Mhe Balozi aliambatana na Afisa Ubalozi Richard M. Lupembe. Sambamba na ziara hiyo, tarehe 6 Julai 2014 Mhe Balozi alikutana na kufanya mkutano na Watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo wadogo wanaoishi Mjini Ndola Zambia.

Katika mkutano huo, Watanzania walikuwa na mengi ya kumweleza Mhe Balozi kupitia risala ambayo ilisomwa na mmoja wa viongozi wa Watanzania hao. Yaliojitokeza katika risala hiyo yalikuwa ni

I) Changamoto wanazozipata wanapoingia nchini Zambia kupitia mpaka wa Tunduma - Nakonde.

II) Taratibu, Kanuni na Sheria za kuishi nchini Zambia.

III) Upatikanaji wa vibali halali vya kuwawezesha kuishi na kufanya biashara Zambia.

IV) Inapotokea tatizo kwa upande wao wamwone nani.

Mhe Balozi alitoa ufafanuzi wa maswali waliouliza na pia alitoa Rai kwa Watanzania hao kuutumia Ubalozi Kwa kuwa Ubalozi ndio Serikali inayowawakilisha hapa Zambia. Aidha alipokea shukrani kutoka kwa Watanzania hao kwenda Serikali ya Tanzania na Zambia Kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali hizi mbili.
Balozi wa Tanzania nchini Zambia,Mhe Balozi Grace Mujuma akiwa kwenye mkutano huo na Watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo wadogo wanaoishi Mjini Ndola Zambia (hawapo pichani).
Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...