Katika dunia ya leo, kama wewe ni mfanyabiashara basi hauwezi epuka ushawishi wa mitandao jamii. Ingawa wengi wetu tumekuwa tukiitumia mitandao jamaa kwa ajili ya mawasiliano pekee, ila kuna mengi yanaweza kufanyika na kusaidia kukuza ufannisi wa biashara yako.
Kwa kulitambua hilo, Dudumizi Technologies LTD inakuletea mafunzo juu ya njia na namna sahihi za kutumia Facebook kukuza na kuboresha Biashara.

Mafunzo haya yatakuwa ya wiki mbili, bila kukuchosha (tukitambua muda ni kitu muhimu kwa mjasiriamali), tutakutumia dondoo (kwa email fupi) iliyojikita moja kwa moja kwenye utendaji. Hivyo, kila siku utapokea email moja inayokufundisha jinsi ya kutekeleza hatua husika. Mwisho wa siku, utakuwa umejijngea uwezo mkubwa wa kutumia Facebook kwa ajili ya biashara yako.

 Pia, washiriki wote watapata nafasi ya kuuliza maswali kwa email kwenda kwa wataalamu wetu kwa muda wote wa mafunzo bila gharama yoyote. Pia washiriki watajumuishwa kwenye muendelezo wa mafunzo ya matumizi mbalimbali IT kwenye biashara kwa Video.

Walengwa: Wamiliki wa biashara wadogo na wa kati
Gharama: Bure, unachotakiwa ni kujiunga tu na fomu ya mlisho wa email chini
Muda wa mafunzo:  July 21 - Agosti 5
Muda wa mwisho kujiunga: July 20
Idadi ya Washiriki: 100
Lugha: Kiswahili
Muandaaji: Dudumizi Technologies LTD

Fomu ya Kujiunga bofya Hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...