Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars
Ally Mayay Tembele (pichani) anawaarifu ndugu, jamaa na marafiki pamoja na jamii ya
Tanzania kwa jumla kwamba email address yake ya maya@yahoo.com
imeibwa na matapeli na kuanza kutumika vibaya (phishing) kwa kudai
kuwa yeye yupo Ukraine na amekumbwa na matatizo hivyo anaomba msaada wa pesa haraka.
Mbaya zaidi, katika email yake hiyo Ally
Mayay Tembele aliwahi kuambatanisha nyaraka nyeti kadhaa ikiwemo pasipoti ambazo wezi hao
wanazitumia kama alama ya uthibitisho kuwa wao ni yeye. Hao jamaa ni wezi na
waongo wakubwa. Msiwape ushirikiano kabisa.
Ukweli ni kwamba Ally Mayay Tembele yupo
Dar es salaam na wala hajasafiri kwenda nje ya nchi hivi karibuni. Hivyo
anaomba yeyoye anayeletewa email hiyo ya mayayt@yahoo.com
aidharau na wala asitoe ushirikiano wowote na hao watumaji. Ni wezi na matapeli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...