Mats Hummels  ameipaisha Ujerumani kwa kichwa na kuizimisha Ufaransa katika uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro leo na kuipeleka nusu fainali. Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 alifunga bao hilo la pekee dakika ya 13, na Ujerumani inayofundishwa na Joachim Low itaelekea Uwanja wa Belo Horizonte kupambana na mshindi wa robo fainal kati ya Brazil na Colombia baadaye  leo. Chini ni mabeseni yenye madonge ya barafu ambayo wachezaji wa Ujerumani walitumia kutuliza joto kali la jiji la Rio de Janeiro kabla ya mchezo wao na Ufaransa. Inaonesha "ndumba" hii imewasaidia leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2014

    Ndio mwisho wao...hawana mpira wowote wa kusonga zaidi ya hapo.....

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2014

    Ujerumani wanawapiga Brazil...wachezaji wawili muhimu wa Brazil tayari wapo nje Silva na Neymar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...