bom 1Mbunge viti maalum Mhe.Catherine Magige kupitia chama cha mapinduzi CCM akimjulia hali Deepak Gupta (25 aliyepoteza mguu wake ) mmoja wa majeruhi wa bomu lililolipuka jana usiku majira ya saa 4 usiku  katika mgahawa wa VAMA Traditional Indian Culture jijini A rusha na majeruhi hao  kukimbizwa katika hospital ya Selian
bom 2Mhe. Mbunge Catherine Magige akimjulia hali mmoja wa majerui katika hospital ya Selian,kushoto ni Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali hiyo kulia ni Dk.Afizay Mkufya.
bom 4Mhe.Mbunge Catherine Magige akiangalia  kwa uchungu namna Deepak Gupta (25 )mmoja wa majeruhi katika bomu ambapo alipoteza mguu wake wa kushoto .
bom7
Mhe.Mbunge Catherine Magige akimjulia hali mtoto Ridtwaik Lwal (13)aliyejeruhiwa mkononi kwa bomu

Mbunge wa viti Maalum kupitia chama cha mapinduzi CCM Mh.Catherine Magige amelaani vikali  tukio la Bomu lililotokea katika mgahawa wa VAMA Tradition Indian Culture  jijini Arusha huku akiitaka serikali kuwachukulia hatua kali kwa wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo

Mh.Magige aliyasema hayo leo katika hospitali ya Selian wakati alipowatembelea majeruhi nane Raia wa Asia waliolazwa katika hospitali hiyo ambapo wengi wa majeruhi waliumia katika maeneo ya miguu,mikono na tumboni hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi kupoteza mguu wake wa kushoto

Magige alisema kuwa kutokana na matukio ya aina hiyo kutokea kwa mfululizo, hali hiyo imesababisha jiji la Arusha kupoteza amani ili hali Tanzania ni Nchi ya Amani'

"Inasikitisha sana kwa kweli matukio kama haya kujirudia rudia inatia hofu sana kwa wakazi wa Arusha pamoa na wageni wanaokuja katika jiji letu"alisema

Aidha alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa vyombo vya dola kufanikisha kukamatwa kwa wale wote wanaohusika na matukio ya uvunjifu wa amani.(Pamela Mollel wa Jamii blog)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2014

    There have to something better than kulaani tu!! Cut the BS, this stuff has to be stopped, and together we can kwa manufaa ya taifa letu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...