Mhe.Mbunge Catherine Magige akimjulia hali mtoto Ridtwaik Lwal (13)aliyejeruhiwa mkononi kwa bomu
Mbunge
wa viti Maalum kupitia chama cha mapinduzi CCM Mh.Catherine Magige
amelaani vikali tukio la Bomu lililotokea katika mgahawa wa VAMA
Tradition Indian Culture jijini Arusha huku akiitaka serikali
kuwachukulia hatua kali kwa wale wote watakaobainika kuhusika na tukio
hilo
Mh.Magige
aliyasema hayo leo katika hospitali ya Selian wakati alipowatembelea
majeruhi nane Raia wa Asia waliolazwa katika hospitali hiyo ambapo wengi
wa majeruhi waliumia katika maeneo ya miguu,mikono na tumboni hali
iliyopelekea mmoja wa majeruhi kupoteza mguu wake wa kushoto
Magige
alisema kuwa kutokana na matukio ya aina hiyo kutokea kwa mfululizo,
hali hiyo imesababisha jiji la Arusha kupoteza amani ili hali Tanzania
ni Nchi ya Amani'
"Inasikitisha
sana kwa kweli matukio kama haya kujirudia rudia inatia hofu sana kwa
wakazi wa Arusha pamoa na wageni wanaokuja katika jiji letu"alisema
Aidha
alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa vyombo
vya dola kufanikisha kukamatwa kwa wale wote wanaohusika na matukio ya
uvunjifu wa amani.(Pamela Mollel wa Jamii blog)
There have to something better than kulaani tu!! Cut the BS, this stuff has to be stopped, and together we can kwa manufaa ya taifa letu
ReplyDelete