Yule Mdau wa Sweden aliyeandika katika blog hii hapo tarehe 8 septemba 2010 aliyeahidi kujenga studio ya kisasa kwa Watanzania, sasa iko tayari huko Sweden. Bado ni kwa Watanzania. 
Mabadiliko ya sehemu ya kuijenga studio hii ni kutokana na hali halisi kuwa Sweden kuna Wataalamu wa aina zote tutakaowahitaji katika kazi zetu kadri wateja wetu watakavyotaka na vifaa muhimu katika kazi zinapatika haraka na kwa uhakika.
 Katika Project hii kuna mambo mengi sana yanayotakiwa kufanyika ili kukidhi kile kilichokusudiwa kwa walengwa (Wasanii wa muziki na filamu) ili kila mmoja akidhi kiu yake. Kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu, kampuni hii inaweza kuja kuwa ni kitengo cha utafiti katika maswala ya sanaa za nchi zinazoendelea na zilizoendelea. 
Nimetafutwa na kuitwa kwa mahojiano. Swali lilikuwa, nadhani ni kwanini kuna utofauti mkubwa kati ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea katika kusambaa na kununuliwa kwa muziki na filamu? Nimeshatoa maoni na ushauri wangu nionavyo kwa Tanzania. Nitajibiwa baada ya miezi kadhaa maana waamuzi sio walionihoji, bali ni watu wengine katika kamati zao za utafiti (EU). 
Tutangulize maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu. Tunaweza kupata utatuzi wa kitaalamu katika swala hili. Tembeleeni www.msolab.se tovuti ya Kampuni yetu MSOL na jitahidini na ninyi wenzangu kui-like MSOL ili kuonyesha kuwa inaungwa mkono na wengi ili tufikiriwe kuwa katika utafiti wao. Lakini mimi maelezo yangu yote nimetilia mkazo zaidi kwa nchi ninayoifahamu vizuri Tanzania. Jamani tutangulize uzalendo. Tanzania kwanza. 
Peters Mhoja /CEO/ MSOL-AB
E-Mail: petersmhoja@hotmail.comKwa mambo yooooooote BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...