Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2014

    Naomba nielezwe tofauti maana baada ya kuangalia video nimeona ananyoa nywele pia.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2014

    Hili swali ni la ankal, huyu kijana ni mtoto wa yule nguli maarufu wa zamani aliekua akilisakata kabumbu na wana T.P Lindanda Kawekamo Pamba ya Mwanza...Khalid Bitebo???duuh jamaa namkumbuka enzi zake kirumba wakati niko kinda alivyokua anawachambua mabeki wa timu pinzani haswa wakicheza Pamba na Yanga...Khalid Bitebo alikua juu huwezi linganisha sijui na kina okwi,na hawa bongo flava chips mayai.
    mdau wa London.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2014

    Wabongo mjifunze kupenda kazi zenu, kazi ni kazi tu, bora mkono uende kinywani, wewe ni KINYOZI, period.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 20, 2014

    Kinyozi ni mnyoaji chini ya mwembe? Hii kali. Kinyozi / berber ni mnyowaji wa nywele ima awe katika duka ( salon) au popote pale. Hayo mambo ya kusafisha nyuso (facial) ni huduma nyinginezo za urembo zinazotolewa na maduka ya kisasa ya unyoaji, usukaji nk. Mfano mkulima ni mtu anayetumia jembe la mkono au plau au trekta. Wote hao ni wakulima ila kuna mkulima mdogo mdogo na mkulima mkubwa lengo lao ni moja japo mazingira ni tofauti. Tuache kujikweza jamani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2014



    Mambo vipi Mdogo wangu Masoud, longtime bro toka mwanza kaluta mtaa maarufu wa vijana rock city. safi sana kwa hatua uliyofikia baabkubwa. Huu ni ushauri wa bure ndugu yangu taulo hazina athari kubwa sana ya maambukizi kwani ni magonjwa tu ya ngozi na unaweza tibu kwa gharama ndogo nadhani ungefikiria zaidi pia kwenye mashine unazotumia pia licha ya sterilizer weka kila star na mashine yake au kit nzima sio ghali maana hii ni long term investment kwani tayari soko unalo hii iwe hatua ya pili. kwenye vitu kama mashine au twizer za kucha hapo ndio hatari ukimwi hauna dawa kuliko hiyo taulo ingawa pia ni hatua bora kwa mbinu za kibiashara wateja wataona umefanya jambo kubwa sana. Angalia sana kwenye swala mashine na vitu vyenye ncha kali.

    keep up the good job Masoud,Nikiwa bongo promise nakuja kunyoa kwako bro.

    Hussein Masha
    UK

    ReplyDelete
  6. Kijana Bitebo, nilikuwa nakusikia tu Ankal Michuzi akikutaja. Nimefurahi kukusikiliza. Naona umeongelea mambo ya msingi sana katika ujasiriamali: ujuzi wa hali ya juu katika shughuli yako, kujiamini, na kuwajali wateja kwa kuwahudumia vizuri na kuwaheshimu.

    Ni ukweli usiopingika kuwa mteja akiridhika na kufurahi, anakwenda kuwa mpiga debe wako. Mimi husoma vitabu mbali mbali, vikiwemo vya mambo ya biashara na ujasiriamali, na hayo ni baadhi ya yale ambayo nimejifunza. Panapo majaliwa, nitakapostaafu, nami nataka kuwa mjasiriamali. Nakutakia kila la heri

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2014

    Mdau Hussein Masha..kumbe upo UK? Duh long time manake enzi zile TP Lindanda huku David Mwakalebela, Abdalla Bori, George MAsatu, Beya Simba, Khalifan Ngassa, Kitwana Selemani, Fumo Felician Chama lilikamilika.
    Paul

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2014

    Wadau naomba tafsiri ya neno hair designer ni mtu anefanya kazi gani? na maana ya neno kinyozi ni mtu anaefanya kazi gani?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2014

    Kijana anaweza kufika mbali akijituma zaidi kiubunifu na kiutaalamu. Kinyozi anaweza kutumia machine,mkasi,kisu cha kiwembe na kukuchonga kufuatana na uzoefu wake. Hair designer anaweza pia kutumia vifaa hivyo
    au si lazima atumie vifaa anaweza
    kusafisha nywele,kuzilainisha kwa Chemicals muhimu na ku-design kufuatana na mapendekezo yake au mteja kwa kuongezea ubunifu wa kisasa sawa na nchi zilizoendelea
    Saloon ya kisasa iwe na ubunifu wa aina zote.Nitakuwa DIASPORA wa kwanza kumtembelea kujiunganisha na masuper stars wetu wakibongo umefanya kazi mzuri kijana uwe mfano mzuri kwa vijana wengine.

    MIKIDADI-DENMARK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...