Viongozi wa ngazi ya juu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kwa mikoa iliyo jirani na Hifadhi za Taifa wanakutana Nashera Hotel kujadili ushirikiano baina yao na Hifadhi za Taifa,(TANAPA) katika kupambana na uhalifu unaolenga Maliasili.
 |
Mgeni Rasmi katika Warsha ya Mashirikiano kati ya TANAPA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Mororgoro Joel Bendera (wa tatu toka kulia) akiwa na viongozi wengine,toka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP, Leonard Paul, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo, Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Allan Kijazi. Wengine baada ya RC Bendera ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikya na mwisho ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifungua warsha ya Mashirikiano baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mikoa iliyo jirani na Hifadhi za Taifa . |
 |
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, (TANAPA) Allan Kijazi akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Mashirikiano kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mikoa inayopakana na Hifadhi za Taifa. Mkutano unaofanyika katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro. |
 |
Mmoja wa washiriki katika Warsha ya Mashirikiano baina ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama na TANAPA, Mrakibu wa Polisi, Mary Lugola akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera mara baada ya kufungua warsha ya viongozi hao . |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...