Na TheHabari.Com
MTANDAO
wa Wanawake na Katiba nchini Tanzania umewakutanisha baadhi ya Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na
Katiba kujadili namna ya kushinikiza masuala ya haki za wanawake
kuingizwa katika rasimu ya pili ya Katiba Mpya.
Semina
hiyo iliyoshirikisha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na
wanahabari imeanza leo katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es
Salaam na itafanyika kwa siku mbili yaani Julai 24 na 25, 2014.
Akizungumza
kukaribisha washiriki wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA,
Valerie Msoka alisema wajumbe katika mkutano huo watajadili umuhimu wa
kuimarisha masuala ya haki za wanawake katika Katiba.
Alisema
kuwa wajumbe pia watajadili namna ya kutetea na kulinda masuala muhimu
ya haki za wanawake yaliyojitokeza katika rasimu ya pili ya Katiba Mpya
ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na masuala
ya katiba yenye maslahi ya wanawake na taifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary
Rusimbi ambao ni moja ya taasisi zilizoratibu mkutano huo, alisema
pamoja na mambo mengine madhumuni ya mkutano huo ni kuwawezesha wabunge
wanawake kwa wanaume katika Bunge Maalum la Katiba na wanaharakati wa
jinsia na haki za wanawake kuimarisha hoja zao.
Katika
mkutano huo wahariri wa vyombo anuai vya habari kwa nyakati tofauti
waliwataka wajumbe hao kuvitumia ipasavyo vyombo vya habari ikiwa ni
pamoja na kutoa ushirikiano ili hoja zao ziingie katika vyombo hivyo na
kuifikia jamii.
Kwa
upande wao baadhi ya wajumbe wa bunge maalum la Katiba wakizungumza
kujibu baadhi ya maswali ya wahariri wa habari walisema wamejipanga
kupaza sauti kuhakikisha hoja zao wanazozipigania zinaingizwa katika
Katiba Mpya.
Naye
Mjumbe wa Bunge Maalum, Dk. Avemaria Semakafu alivitaka vyombo vya
habari kuendelea kuwaunga mkono wanamtandao hao ili kupigania kero za
akinamama na wananchi kwa ujumla na kuhakikisha zinapata majibu katika
mchakato wa uundaji katiba mpya.


Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi
akiwasilisha mada katika katika mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.

Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Ruth Meena akiwasilisha mada.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...