![]() |
Marehemu Henry Lymo maarufu kama Kipese. |
Na Dixson Busagaga
TASNIA ya Habari na michezo mkoani Kilimanjaro imepata pigo kufuatia kifo cha ghafla cha Mtangazaji wa kituo cha radio cha Moshi FM Henry Lyimo, maarufu kama Kipese. Marehemu Kipese amefariki dunia usiku wa jana akiwa njiani akitokea Rombo katika eneo la njia Panda, Himo, baada ya pikipiki aliyokuwa akitumia kugongana na pikipiki nyingine.

Taarifa za awali zinasema Marehemu
Kipese alikuwa akitokea wilayani Rombo ambako amekuwa akifanya
shughuli zake na kwamba wakati anarejea ndipo mauti yakamfika baada ya
kuumia vibaya katika ajali hiyo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kilema wilayani Rombo kungojea taratibu nyingine toka kwa ndugu zake.
Tayari makundi mbalimbali ambayo
marehemu amekuwa karibu nayo kwa shughuli za kikazi yametoa taarifa za
masikitiko kufuatia kifo cha Kipese huku yakipanga kukutana asubuhi
hii kwa ajili ya kupanga mambo mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha
mazishi hayo.
Kundi la kwanza ni kundi la waandishi
wa habari mkoa wa Kilimanjaro kupitia klabu yake ya Media Club of
Kilimanjaro wamepanga kukutana asubuhi hii katika eneo la
Posta. Kundi la pili ni la wafanyakazi wote
wa Moshi FM radio ambako marehemu alikuwa akifanya kazi hadi Mauti
yanamkuta wamepanga kukutana asubuhi hii kuanzia majira ya saa
2.
Kundi la tatu ni la wadau wa michezo
mkoani Kilimanjaro ambako licha ya kwamba Marehemu Kipese alikuwa
mtangazaji wa kipindi cha Michezo katika radaio aliyokuwa akifanyia
kazi pia alikuwa mwamuzi wa mchezo wa soka. Wadau hao wamepanga kukutana katika
ofisi za chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) kujadili namna ya
kushiriki msiba huo mzito kwa tasnia ya habari na
michezo.
Globu ya Jamii inaungana na famili, ndugu jamaa na marafiki wa marehemu katika kuomboleza msiba huu mzito.
Globu ya Jamii inaungana na famili, ndugu jamaa na marafiki wa marehemu katika kuomboleza msiba huu mzito.
Matokeo ya Utafutaji
Inna Lillahi Wa Inna Ilahi Raaji'oon
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...