Msimamizi wa Uchaguzi Bw. Alfred Kayombo (kulia) akimtangaza mshindi wa nafasi ya mwenyekiti Bw. Ibrahim Ngogo.
Kwa mara ya kwanza katika historia, chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimefanya uchaguzi wa uongozi mbalimbali ambapo Bw. Ibrahim Ngogo amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa ngazi ya wilaya.

Na Edwin Moshi, Makete
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Alfred Kayombo amesema Bw. Ibrahim Ngogo amepata kura 25 akifuatiwa na Isaac Sanga aliyepata kura 6 na Shaaban Mkakanze aliyepata kura 1.
Bw. Kayombo amesema kutokana na umuhimu wa demokrasia ndani ya chama hicho, wameamua kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza toka chadema iingie wilayani hapa, hivyo kuonesha kuwajali wanachama wake
Mbali na viongozi hao wa juu wa chama pia Bw. Lazaro Chaula amechaguliwa kuwa katibu mwenezi wa Chadema wilaya ya Makete kwa kupata kura 30, Bi. Rose Mbilinyi amechaguliwa kuwa Mtunza hazina wa wilaya kwa kupata kura 26.
Aidha Bw. Atukuzwe Mahenge amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) wilaya na Bw. Shadraack Mwachota akichaguliwa kuwa katibu wake na wote wamepita bila kupingwa.
Bi. Beatrice Kyando amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema wilaya (BAWACHA), Bi Christina Timoth akichaguliwa kuwa katibu wa BAWACHA, na Bi. Mariam Asheli akichaguliwa kuwa Katibu wa uhamasishaji wa BAWACHA na wote wamepita bila kupingwa.
katika uchaguzi huo pia Bw. Abiud Elia amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee kwa kura 3, Abeli Juma Sanga akipata kura 1 na kuchaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti, pamoja na Simon Nyasanga kuwa katibu wa baraza la wazee wilaya.
Katika hatua nyingine wamechaguliwa wajumbe 4 waliochaguliwa kuingia kwenye kamati tendaji ambao ni John Sanga, Patison Pela,Orignal Sanga na Alafat Msigwa, huku Bw.Illomo Werner Naftal akichaguliwa kuwa mwakilishi wa wilaya kwenye mkutano mkuu taifa.
Akiahirisha mkutano huo mwenyekiti wa Chadema wilaya Bw. Ibrahim Ngogo amewasihi wajumbe kuondoa makundi na kutokubali kutumia kwa ajili ya kukibomoa chama na badala yake washikamane wawe kitu kimoja kukijenga chama.
"Makamanda uchaguuzi umeisha haitakiwi tuwe na makundi, tushikamane kukijenga chama chetu, hilo ndilo la msingi kwa sasa, sisi viongozi mtupe ushirikiano" amesema Ngogo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...