Mwanamfalme Akishino
Mwanamfalme Akishino wa Japan na Mkewe wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 02 Julai, 2014 kwa ziara rasmi ya siku tano.

Akiwa hapa nchini Mwanamfalme Akishino atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kutembelea Kituo cha Mafunzo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO); Makumbusho ya Taifa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akiendelea na ziara yake, Mwanamfalme Akishino atatembelea Visiwa vya Zanzibar na kufanya mazungumzo na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kutembelea eneo la Mji Mkongwe na hatimaye kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Mbuga ya Wanyama ya Serengeti.

Aidha, katika siku ya mwisho ya ziara yake Mwanamfalme Akishino atatembelea Banda la Japan kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba.

Mwanamfalme Akishino ambae ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa Mfalme Akihito anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 06 Julai, 2014 na kuondoka siku hiyo hiyo kurejea nchini kwake.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
01 JULAI, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...