Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.

Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Libya jijini Dar es salaam. 

Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini. Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa alikwisha kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho.

Maiti imehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.

IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam
Julai 2,2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2014

    INA LILAHI WAINA ILAYHI RAJIUN

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2014

    Msongo wa mawazo au nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...