Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC wakipata maelezo kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw. Boscow R. Mabena.
Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kikundi cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya matumizi ya makaa ya mawe majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa kutumia majiko maalum baada ya kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa matumizi ya majumbani. Mbalawala kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.
Majiko maalum yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia majumbani.
Mtaalam wa Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena akitoa maelezo namna ambavyo Coal Briquett Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka hali yake ya mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango, (wa tano kutoka kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine ni viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL inayojishughulisha na uchimbaji wa makaa ya mawe. 
Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa makaa ya mawe. Kampuni ya TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya Mawe Ngaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2014

    Ngaka ipo wilaya gani, Mkoa upi Tanzania?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...