Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ( wa pili kuli) Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa (katikati) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkititi wa ‘Masjidil Huda’ na Swala ya Ijumaa uliofanyika leo Julai 4, 2014, Chamaz jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wenyeji wake wakati alipowasili Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa msikiti huo uliofanyika leo Julai 4, 2014. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokelewa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, wakati alipowasili Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa msikiti huo uliofanyika leo Julai 4, 2014. Picha na OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...