Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi, Bi. Monica Mwamunyange akibadilishana kadi na Profesa Liu Xueyi
kutoka Chuo kikuu cha Southwest Jiatong, wakati mkufunzi huyo na wanafunzi wa
chuo hicho walipotembelea wizara ya Uchukuzi leo mchana kujifunza na
kubadilishana uzoefu katika masuala ya reli hasa reli ya mwendo kasi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi, Bi Monica Mwamunyange, akifafanua jambo kwa Wakufunzi na wanafunzi
wanaochukua shahada za Uzamili na Uzamivu katika Reli kutoka Chuo Kikuu cha
Southwest Jiatong, wakati walipotembelea Wizarani hapo kujifunza na
kubadilishana uzoefu hasa kwenye usafiri wa Reli, leo mchana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi, Bi Monica Mwamunyange (wa nne kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja
na wakufunzi, wanafunzi na sehemu ya wakurugenzi wa Wizara ya Uchukuzi, wakati
wanafunzi hao wanaochukua shahada za uzamili na uzamivu katika Eneo la Reli
kutoka chuo kikuu cha Southewest Jiatong walipotembelea Wizarani hapo leo mchana
ili kubadilishana uzoefu hasa katika treni za mwendo kasi. Aidha chuo hicho kimeahidi
kubadilishana uzoefu na Chuo che Reli Tabora ili kujenga uwezo katika masuala
ya Reli. (Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...