Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameandaa futari kesho (Julai 17 mwaka huu) kwa wadau mbalimbali wa mpira wa miguu.

Shughuli hiyo itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo waalikwa wataanza kuwasili saa 11.30 jioni.

Waalikwa katika futari hiyo wametoka katika makundi mbalimbali. Makundi hayo ni wadhamini, klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza za Dar es Salaam ambazo zitawakilishwa na watu wawili wawili.

Viongozi wa zamani wa TFF, Said El Maamry, Leodegar Tenga, Muhidin Ndolanga, Athuman Nyamlani, Mwina Kaduguda, Michael Wambura, Fredrick Mwakalebela na Ashery Gasabile. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliopo Dar es Salaam, Wizara ya Michezo na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Vyama shiriki; TWFA, TAFCA, TASMA, SPUTANZA, FRAT ambavyo vitawakilishwa na watu watatu watatu, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Baraza la Michezo la Taifa (BMT), wahariri wa habari za michezo, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na Polisi kanda Maalumu- Dar es Salaam.

Wajumbe wa kamati ndogondogo za TFF waliopo Dar es Salaam, wazee wa Simba na Yanga- watano kutoka kila klabu, timu ya Serengeti Boys, klabu ya Saigon, Bodi ya Ligi Kuu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wakuu wa wilaya za Dar es Salaam, wabunge wa Dar es Salaam, Meya wa Dar es Salaam, Meya wa Kinondoni, Meya wa Ilala na Meya wa Temeke.

Waalikwa wengine ni Omari Abdulkadir, Amin Bakhresa, Harudiki Kabunju, Hamis Kissiwa, Ismail Aden Rage, Masoud Sanani, Jamal Bayser, Hassan Dalali, Imani Madega na Mbaraka Igangula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2014

    Ftari inasaidia kuwaunganisha watu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...