MWL.ERNEST MWAMKAI KIONDO
1932-2014
1932-2014
Familia ya Mwl.Ernest Mwamkai Kiondo ya Dar es Salaam, Ambanguru, Mlalo, Korogwe na kwaminchi Tanga .
Kwa heshima na taadhima kuu tunapenda kutoa shukran zetu za dhati kwa ndugu,majirani, jamaa na marafiki wote ambao kwa namna moja au nyingine waliweza kushiriki katika msiba, wa Baba yetu mpendwa aliefariki Tarehe 22 May 2014 katika Hospital ya TCHC ,Tanga (TANGA CENTRAL HEAKTH CENTER) na kuzikwa katika makaburi ya Bombo ,Tanga Tarehe 25 May 2014.
Tumefarijika sana pia kwa wale wakiosafiri masafa marefu toka sehemu mbali mbali Nchini na nje ya Nchi walitupa moyo wa Upendo tulipokuwa nao na faraja nyingi tulizipata toka kwa watu mbali mbali waliotuma salaam za rambirambi toka sehemu mbali mbali duniani.
Haitakuwa rahisi kwetu kuwataja na kuwashukuru kila mmoja wenu ingawa tulipenda sana iwe hivyo, tunaomba kwa tangazo hili wote mtukubalie na mpokee shukrani zetu za upendo toka kwetu.
Hata hivyo familia inapenda kutoa shukran za pekee kwa waliochangia kutoa Huduma ambayo milele itabaki katika nyoyo zetu ,nao ni madaktari na manesi wa hospitali ya TCHC hususan DR.Gila na DR.Patrick kwa jitihada zao kuu za kumtibu baba yetu mpendwa.
Pia tunapenda kuwashukuru wanajumuiya wote wa kanisa la nguvumali la Mtakatifu Yohana krisostomom wa Nguvumali ,Tanga ,Baba Askofu Mahimbo William Mndolwa alieongoza misa ya mazishi hayo na Padre kiongozi wa kanisa Isack Nogea, Baba wa kiroho wa baba yetu na Father Paulo lihinga. Tunawashukuru sana .
Pia tunawashukuru viongozi wote wa mkoa wa Tanga uliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa ndugu Salum M. Chiwa kwa kushirikiana nasi katika msiba huo.
Mwisho tunapenda kuwajulisha kuwa tutahitimisha msiba wa baba yetu kwa kukesha nyumbani kwake Kwaminchi mjini Tanga siku ya ijumaa Tarehe 4 july 2014 na kufuatiwa na misa jumamosi tarehe 5 july 2014 saa tano asubuhi katika kanisa la mtakatifu Yohana krisostomom, Nguvumali,Tanga.Wote mnakaribishwa
Asanteni sana.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
AMEN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...